Ripoti ya Utafiti ya Timu ya Kimataifa ya watafiti iliyochapishwa kwenye jarida la tiba la The Lancet, inaonyesha zaidi ya watu milioni 39 wanaweza kufa kutokana na usugu wa dawa za Antibiotiki.

Utafiti huo, ambao ulijikita zaidi kwenye usugu wa dawa hizo, umekadiria kwamba watu milioni 1.91 wanaweza kufa kutokana na changamoto hiyo ifikapo mwaka 2050, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 kwa mwaka, ikilinganishwa na mwaka 2022.

Kufuatia hali hiyo, Wataalamu hao wa Kimataifa wanasema wakati umewadia wa kuchukua hatua madhubuti, ili kuwalinda watu ulimwenguni, kutokana na hali hiyo inayosababishwa na usugu wa dawa zinazotumika kutibu maambukizi.

Itakumbukwa kuwa ripoti ya awali ilionesha kuwa zaidi ya watu milioni 1 walikufa kutokana na usugu wa dawa kote ulimwenguni kila mwaka, kuanzia mwaka 1990 hadi 2021.

Tetesi za Usajili Duniani leo 17 September 2024
Msifuate mkumbo Barabarani - Mufti