Waziri wa Afya wa Lebanon, Firas Fabias amethibitisha vifo vya Watu wasiopungua tisa, baada ya kutokea kwa mlipuko wa vifaa vya mawasiliano.
Amesema katika mlipuko huo, uliotokea kwenye maeneo kadhaa ya Lebanon hasa yanayodhibitiwa na Wanamgambo wa Hezbollah, watu wasiopungua 2,750 wamejeruhiwa na zaidi ya 200 wana hali mbaya.
Hezbollah nayo imesema wapiganaji wake wawili pia wamefariki na wengine wamejeruhiwa nchini Syria ambako pia kumetokea milipuko kama huo.
Tayari Umoja wa Mataifa – UN umeonya juu ya kitisho cha kusambaa kwa mzozo kati ya Israel na Hezbollah, kufuatia tukio hilo linalongeza wasiwasi, ambalo limetokea katika mazingira tata.