Jeshi la Polisi Nchini, limewataka Wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuwa aliyekuwa Meya wa Ubungo na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Boniface Jacob ametekwa bali wanamshikilia kwa tuhuma za makosa ya kijanai.

Taarifa  iliyotolewa hii leo Septemba 18, 2024 na Msemaji wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi  David Misime imesema wanamshikikia Kada huyo mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi Jijini Dar es Salaam kutokana na makosa anayotuhumiwa nayo.

Tayari Wakili Hekima Mwasipu wa CHADEMA amethibitisha kukamatwa kwa Boniface na kudai kuwa amepelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Amesema, “anatuhumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo.”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 19, 2024
Dkt. Mwinyi: Utekelezaji wa Miradi uzingatie wakati