Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezishauri taasisi za dini kushirikiana na taasisi za Serikali na binafsi kukemea maovu yote ndani ya jamii.

Rais Alhaj Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo alipozungumza Katika Baraza La Maulid Ukumbi wa Idrissa Abdul Wakil Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema, suala hilo sio la kuachiwa taasisi au mtu mmoja bali ni wajibu kushirikiana kukabiliana na maovu hayo kwa pamoja.

Aidha, amewasisitiza wananchi kuendelea kushikamana na na kupendana kuepuka mifarakano ili kujenga nchi na kuleta Maendeleo ya haraka.

Akizungumzia suala la maadili ya usomwaji wa Maulid Dkt. Mwinyi amelishauri Baraza la Maulidi kwa kushirikiana na Afisi ya Muft kutoa maelekezo na miongozo kupitia wanazuoni wa ndani na nje ya nchi kurejesha misingi sahihi ya kimaadili.

Kwa upande mwingine Rais Alhaj Dkt. Mwinyi amewaasa Waislamu kufuata maelekezo na mafunzo ya Mtume Muhammad (SAW) Ili kudumisha Amani ikiwemo kupendana.

Mchengerwa atoa maagizo ujenzi Longido Samia Girls
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 19, 2024