Chelsea wako tayari kumruhusu winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, huku klabu ya Ufaransa ya Marseille ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (TeamTalks),

Arsenal wameanza mazungumzo ya kandarasi na beki wa kati Gabriel Magalhaes, 26, ingawa mazungumzo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil yako katika hatua za awali. (Football Insider),

Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen alihusishwa na kuondoka Manchester United msimu uliopita, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, anasema hakufikiria kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Mail),

.

Mshauri wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic amewasiliana na meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic, huku meneja wa timu hiyo ya Serie A Paulo Fonseca – ambaye aliteuliwa msimu wa joto – tayari akiwa chini ya shinikizo baada ya kuanza vibaya msimu. (Sky Sports Ujerumani)

Rais wa Inter Milan Guiseppe Marotta anasema klabu hiyo ilikuwa karibu kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 24, alipokuwa na umri wa miaka 15, kabla ya mpango wa uhamisho huo kuharibika (Soka Italia),

Beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell bado anatarajiwa kuondoka Chelsea mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kurejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza baada ya kushindwa kupata uhamisho msimu wa joto. (Football Insider)

.

Chelsea inaweza kumteua Sachin Gupta, ambaye ni makamu wa rais mtendaji wa shughuli za mpira wa vikapu kwa upande wa NBA Minnesota Timberwolves, kuhudumu katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Athletic – Subscription Required),

Newcastle United wanamfuatilia beki wa kulia wa Chelsea Josh Acheampong mwenye umri wa miaka 18 na wanaweza kujaribu kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 19. (gazeti – Subscription Required).

Feisal awaingiza vitani GSM,MO DEWJI NA BAKHRESA
Malimwengu: Anapokea siri, ataitoa msibani siku ukifa