Siku za hivi karibuni kumeibuka taarifa za mchezaji wa Azam FC Feisal Salum Fei Toto, kuhitajika na vilabu vikubwa ndani na nje ya nchi ikiwemo Mamelod Sundowns.

Kwa vila vya ndani ni Simba na Yanga wote wanaivizia tena saini ya Fei Toto, kwa upande wa Yanga ni wanafikiria namna ya kumrudisha tena mchezaji huyo.

MKATABA WA FEI TOTO UKO HIVI.

Mkataba wa Fei Toto na Azam una kipengele cha kuvunjwa kwa $500,000 (Tsh 1,362,220,000 ) ndani ya miaka miwili ya kwanza.Lakini ifikapo mwishoni mwa msimu huu thamani ya mkataba huo itapungua hadi $250,000 (tsh 681,110,000).

Hivyo timing ya vilabu vingi iko pale mwishoni mwa msimu ambapo tsh 600m itatosha kuvunja mkataba wa Fei.Lakini pia Azam wanapambana kumuongezea mkataba mpya ili waendelee kuwa na power juu yake.

VITA YA MATAJIRI

Mkataba wa Feisal Salum na Azam umebakia miaka miwili na Yusuf Bakhresa amevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo tangu ajuunge klabuni hapo msimu uliopita hivyo anataka kufanya maboresho ya mkataba wa Fei.Taarifa zinasema upande wa mchezaji unataka mshahara wa milioni 70 kwa mwezi jambo linaloweza kufanywa na Azam fc.

Klabu ya Simba imekuwa ikimwinda Feisal tangu akiwa na Yanga,walishindwa kumsajili nyota huyo kutokana na mikataba migumu aliyokuwa nayo na Azam FC . Kwa sasa nyota huyo yupo Azam hivyo Simba wanaweza kufanya mazungumzo na Azam na kumaliza biashara kama watakubaliana. Mo Dewji amekuwa akifurahishwa na uwezo wa mchezaji huyo na anaweza kulipia gharama zote zinazotakiwa.

GSM ni kama wamerudisha mahusiano mazuri na mchezaji huyo baada ya kuwa na uelewano mzuri baina ya Feisal na Rais wa Yanga Eng.Hersi Said. Nyota huyo amekiri hana tatizo na Yanga na kama watamuhitaji basi wamalizane na Azam. Huu ni wakati mzuri kwa Feisal Kutajirika ,anapaswa kuchanga karata zake vyema baada ya kuwashika matajiri wote watatu.

Mkude afunguka bifu lake na Aucho
Tetesi za Usajili Duniani tarehe 19 septemba 2024