Manchester City wako mbioni kumsajili Mjerumani Jamal Musiala, 21, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Real Madrid kwa kiungo huyo wa Bayern Munich. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin hajakaribia kusaini mkataba mpya zaidi ya msimu ujao na Everton, huku Newcastle United ikiendelea kufuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (CaughtOfisde)

Mkataba wa mlinzi wa Liverpool Trent Alexander-Arnold unakamilika msimu ujao na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25, anasema kushinda mataji itakuwa sehemu muhimu ya mawazo yake linapokuja suala la kusaini nyongeza ya kandarasi. (Liverpool Echo)

Trent Alexander-Arnold
Mkatabda wa mchezaji wa Liverpool Trent Alexander-Arnold unakamilika msimu ujao

Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham wote zinavutiwa na mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26. (Teamtalk)

Newcastle ndio klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi ya Premia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa chini ya miaka 21 mzaliwa wa Marekani wa Italia Luca Koleosho, 20, ambaye pia anawaniwa na klabu ya Burnley. (HITC)

Ligi ya Premia, pamoja na ligi kuu za Ulaya, zinajaribu kukubaliana mpango ambao utamaanisha kuwa usajili ujao wa majira ya joto utafungwa kabla ya kuanza kwa msimu. (Mirror)

Kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter angependa kujiunga na Everton ikiwa nafasi itapatikana. (Football Insider)

Real Madrid wanamfuatilia mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Castello Lukeba, 21. (Marca – kwa Kihispania)

Aston Villa, Fulham na Nottingham Forest wanamfuatilia winga wa Galatasaray, 24, Baris Alper Yilmaz, wakati Forest, Brighton na Tottenham wanamnyatia mshambuliaji mwenza wa Uturuki Semih Kilicsoy, 19, ambaye yuko Besiktas. (CaughtOffside)

Wasaka vipaji wa Manchester United, Newcastle na Tottenham walifuatilia mechi ya Jumamosi ya Southampton ambapo kiungo wa kati wa Uingereza Tyler Dibling, 18, aliifungia klabu hiyo. (HITC)

CAF:Waarabu wafanyiwa Ubaya Ubwela
Hakuna anayetaka kukutana na Yanga makundi ya CAF