Klabu ya Azam FC imeendelea kufanya vyema ligi kuu ya NBC baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Coastal Union. Bao hilo la Azam liliwekwa kimiani na Nassor Saadun dakika ya 9 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo . Ushindi huo wa Azam unawafanya kufikisha alama 8 katika michezo 4 waliyocheza wakipanda mpaka nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi.
Azam Chini ya Kocha Rachid Taousi imekuwa ikifanya vyema baada ya kucheza michezo 3 ikishinda 2 na sare moja wakifunga jumla ya mabao 5 pasipo kuruhusu bao lolote kutikisa nyavu zao. Nyota wa mchezo huo aliibuka Nassor Saadun kutoka Azam FC .
Coastal Union kuuza ukwaju Buguruni
Kabla ya Mchezo dhidi ya Azam msemaji wa Coastal Union alinukuliwa akisema ”Kama Azam wataibuka na ushindi wa mchezo huo basi wachezaji na viongozi wa Coastal Union wataanza kuuza ICE CREAM maeneo ya Buguruni”, Msemaji huyo aliongeza kwa kusema ”Tuna timu nzuri zaidi ya Azam FC na tutafanya kweli kwenye huu mchezo”