Klabu ya Simba imefanikiwa kumsajili kiungo wa zamani wa AS Vita na timu ya taifa ya  Congo  Ellie Mpanzu. Kiungo huyo aliwasili nchini siku chache zilizopita akitokea Ubelgiji alikokwenda kufanya majaribio katika klabu ya Genk na mambo hayakwenda sawa. Simba walikuwa na uhitaji wa winga huyo tangu msimu uliopita na sasa wamefanikiwa kupata saini yake.

Nyota huyo amejiunga na Simba na ataanza kuitumikia klabu hiyo mwezi Oktoba kwenye michuano ya Shirikisho na mwezi januari wakati wa dirisha dogo litakapofunguliwa atacheza ligi kuu ya NBC pamoja na mechi za kombe la CRDB, kwa sasa atajiunga na kambi rasmi ya timu hiyo iliyoko Bunju kwa ajili ya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kuelekea msimu mpya wa kombe la shirikisho. Ujio wa Mpanzu utawaweka rehani wachezaji watatu wa kigeni ambao ni Ayoub Lakred anayesumbuliwa na majeraha,Steven Mukwala na Kiungo Fabrice Ngoma aliyekosa nafasi chini ya Kocha Fadlu.

Taarifa za ndani zinasema nyota huyo amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu na mshahara wa nyota huyo utakuwa mkubwa kulinganisha na wachezaji wengi wa kigeni.

Hivi ndivyo Mpanzu alivyosaini Simba akiwa na Try Again ,Bw.Hosea ambaye ni mwanasheria wa Simba SC na muwakilishi wa Elie Mpanzui

Mbowe, Bintiye wakamatwa na Polisi
Polisi wamemkamata Lissu wameondoka naye - CHADEMA