Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Kufuatia ugumu wa upatikanaji wa huduma za kibingwa katika maeneo mengi nchini hususan kwenye hospitali za Halmashauri Wananchi Mkoani Manyara wameomba kudumishwa kwa utaratibu wa kambi ya madaktari Bingwa wa Mama Samia, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Kauli hiyo ya Wananchi imekuja kufuatia uzinduzi wa huduma za kibingwa kupitia Madaktari bingwa wa Mama Samia ambayo itatolewa Mkoani humo kwa siku sita katika Hospitali za Halmashauri saba za mkoa huo.

Kambi hiyo, imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emanuela Kaganda ambaye amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa ndani ya muda uliopangwa.

DC Daganda akimjulia hali mtoto aliyefika kuonana na Madakta Bingwa.

Rais Samia atembelea Makumbusho Vita vya Majimaji
Nyota wa Simba awa gumzo MBuni FC