Washitakiwa wanne wa kesi ya kubaka kwa kundi na kumlawiti binti mkazi wa eneo la Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, wamekutwa na kesi ya kujibu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Zabibu Mpangule Washtakiwa watatakiwa kujitetea Septemba 25 na 26, 2024.

Watalazimika kujitetea kufuatia upande wa Jamhuri kuleta vielelezo 12 na mashahidi 18, ambao walitoa ushahidi kuhusu kesi inayowakabili.

Washtakiwa hao ni Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo, Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson na Amin Lema.

Mradi TACTIC kutoa huduma bora kwa Wananch
Mahundi: Fanyeni kazi kwa manufaa ya Nchi, EAC