Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Adolf Ndunguru ameongoza kikao Kazi cha Kamati ya Uendeshaji ya Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Katika Majiji na Miji kwa Kuhusisha Ushindani (TACTIC), Jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la mradi wa TACTIC ni kuboresha usimamizi wa ukuaji wa Miji pamoja na kuziwezesha Halmashauri za Miji na Majiji kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mradi huu utagharimu kiasi cha Dola za Marekani Milioni 410 kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Beki ya Dunia na unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka Sita (6) kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023.

Utekelezaji wa Mradi huu unafanyika kwa awamu kwa kuzingatia makundi haya matatu ya Tier 1 (Mwanza CC, Mbeya CC, Arusha CC, Dodoma CC, Ilemela MC, Morogoro MC, Kahama MC, Kigoma Ujiji MC, Songea MC, Sumbawanga MC, Tabora MC and Geita TC).

Tier 2 (Tanga CC, Moshi MC, Kibaha TC, Iringa MC, Bukoba MC, Singida MC, Bariadi TC, Shinyanga MC, Musoma MC, Lindi MC, Mpanda MC, Njombe TC, Mtwara Mikindani MC, Babati TC and Njombe TC

Tier 3 (Kasulu TC, Tunduma TC, Vwawa TC, Ifakara TC, Makambako TC, Masasi TC, Nanyamba TC, Handeni TC, Bagamoyo DC, Mafinga TC, Tarime TC, Chato DC, Bunda TC, Mbinga TC, Mbulu TC, Nzega TC, Kondoa TC and Newala TC).

Makundi haya matatu yalipangwa kwa kuzingatia takwimu za idadi ya watu kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa miji husika, na mgawanyo wa fedha ulizingatia makundi haya pia.

Ataka mapendekezo ushughulikiaji mmomonyoko wa maadili
Akina Nyundo wakutwa na kesi ya kujibu