Tunarejelea utaratibu wetu na leo nakutana na Mursi (Mun jinsi) kama ambavyo wao wanatamka, hili ni kabila la Surmic linalopatikana nchini Ethiopia.

Watu hawa wanaishi katika eneo la Debub Omo Kusini, karibu na mpaka na Sudan Kusini ambapo kwa mujibu wa sensa ya kitaifa ya mwaka 2007, kuna Wamursi 11,500.

Inaarifiwa kuwa, 848 kati yao wanaishi mijini na jumla ya idadi hiyo, asilimia 92.25 wanaishi katika maeneo ya Kusini mwa Taifa hilo.

Taratibu za Kabila hili la Mursi ni ya kushangaza, wana kitu kinaitwa Bamba la mdomo ambacho hubeba maana kadhaa wakikata midomo na kuvika bamba hilo (sahani) zenye ukubwa tofauti.

Wanasema maana ya kwanza huwa ni ishara ya uzuri au uli.bwende au utanashati, pili ni alama ya kujitolea kwa mume kwa sababu huvaliwa kwa fahari kubwa wakati wa kumpa chakula.

Halafu Mume akifa, bamba la mdomo huondolewa kwa kuwa urembo wa nje wa mwanamke unasemekana kufifia baada ya kifo chake.

Mwisho, bamba ni alama yenye nguvu inayoonekana kwa utambulisho wa Mursi kwani bila hivyo, wanaendesha hatari ya kudhaniwa kuwa mtu wa kabila lingine.

Mimi kusema kweli sipingani na tamaduni za watu lakini nadhani huu ni ukatili na unyama, na hapa ndipo ninapokubaliana na yule Mhenga aliyesema ‘UKITAKA UZURI SHARTI UDHURIKE’ …. Mwamba apewe maua yake.

Maisha: Dawa ya kumtuliza mume ndani ya ndoa hii hapa
Ataka mapendekezo ushughulikiaji mmomonyoko wa maadili