Faudhia Simba – Dar24 Media

Anaitwa Leonard da Vinci, yeye ni raia wa Italia aliyezaliwa April 15, 1452 katika mji wa TuscanĀ  akijipata unaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake cha sanaa ya uchoraji, licha ya kwamba alikuwa na vipaji vingi vya kuzaliwa.

Hata hivyo alitambulika pia kwa mambo mengi kutokana na uhodari wake katika somo la kukokotoa yaani Hisabati, Uhandisi, Sayansi na hata ugunduzi wa mambo mbali mbali.

Moja ya kazi kubwa ambayo ilimtambulisha kiasi kwamba hadi leo imebaki ikizunguziwa midomoni mwa watu, ni picha aliyoichora karne ya 16 ya Monalisa ambaye ni mke wa Mfanyabiashara maarufu, Francesco del Giocondo.

Picha hiyo, iliacha maswali mengi kwa jamii hadi leo hii na ilinunuliwa na Mfalme Francis wa Ufaransa katika miaka ya 1500 kwa kilo 13 za dhahabu, sawa na Dola 650,000 za Kimarekani.

Maswali mengi ambayo yapo kwenye picha hiyo bado ni fumbo kwani sura ya mwanadada huyo inaonekana kwa tafsiri mbili ya kike na ya kiume na pia haikufahamia iwapo alifurahi au alikuwa na huzuni.

Nyusi zake zilikuwa hazipo wengine kusema ilikuwa si swa kwa kipindi hicho kwani Wanawake hawakutakiwa kuonekana nazo, lakini pia uso wake na macho vilionekana kwa upana zaidi.

Leonard da Vinci hakutoa majibu na hakuna ajuaye na sina uhakika kama kuna mtu alidadisi mpaka alipofariki Mei 2, 1519 kwani hakuna anayejua ukweli kuhusu muonekano wa nje wa picha hiyo ya Monalisa hadi leo.

Sasa kwenye fumbo la picha hii ya Monalisa linaakisi fumbo ambalo fundi wa soka na kiungo Bora hapa nchini Feisal Salum (Fei toto), amelitoa na kuzusha maswali lukuki kwa wapenda soka na jamii.

Fei Toto hivi karibuni alisikika akisema kama ikitokea anatakiwa kurudi tena timu yak ya zamani Yanga basi yupo tayari kurejea, kitu kinachopingana na kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba, hatorudi Tena Yanga hadi pale Rais wa Timu hiyo Injinia Hersi atoke.

Feisal anazusha maswali zaidi pale ambapo anasema huwa anaongea vizuri na Injinia Hersi na huwa anamshauri kiasi watu wakabaki midomo wazi.

Ni Feisal huyu huyu ambaye Wananchi walimuamini sana lakini aliwavunja moyo aliposema kuwa anakula Ugali na Sukari na hawezi kurejea Yanga kiasi mpaka Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliingilia kati suala hili kwa kuotaka Yanga imalizane na iache kulumbana na ‘katoto kadogo’.

Upendo wa Yanga kwa Feisal ulinionesha wazi kuwa hawapo tayari kumuachia mchezaji huyo na wengi waliongea vibaya kuhusu Yanga lakini leo hii naweza waelewa Yanga kwamba waligundua mchezaji wao huyo hajajua nini anataka na kauli ya Rais ilisaidia kumaliza sakata hilo.

Feisal wa pichi sio yule ambaye alisikika kutaka kutoka yanga kwa kiwango chake kilichokuwa bora sana chini ya kocha Nabi na mara nyingi alionekana kufanya matokeo pale Wananchi walipozidiwa na ubora wake bado umedumu mpaka leo hii.

Hili linajidhihirisha wazi kwani bado hakuacha kukipiga vizuri hata pale alipotoka yanga kuelekea Azam chini ya kocha Dabo na kiwango chake kiliendea kuwa bora zaidi na kumaliza msimu wa ligi akiwa na magoli 17.

Msimu huu ameanza vizuri pia kwa Fei Toto tayari amechukua tuzo ya mchezaji Bora kwenye mtanange kati ya Azam dhidi ya KMC ambao walipata ushindi wa goli 4-0 na kutoa ishara kuwa rasmi wameanza ligi kwa ushindi huo wa mchezo wa kwanza kushinda.

Kwa ubora wake, ni wazi kuwa anaweza kucheza soka kokote Afrika na haya nje ya Afrika na ndio maana hakuna Timu ambayo haitamani kuwa naye na Wananchi wanaonesha kuwa wapo tayari kumpokea tena kijana wao.

Msemaji wa Yanga, Ali kamwe akalivalia njuga jambo hili kuwataka mashabiki wa Yanga kumsamehe na ‘kumfollow’ tena kijana wao katika mitandao ya kijamii.

Feisal Salum ama Fei Toto anawapa mashabiki wake maana halisi ya kutojua nini anataka na sura yake halisi hasa ni ipi kwa akisi ya picha ya fumbo aliloliacha Leonard da Vinci kiasi inakuwa ni ngumu kupatia jibu kwa haraka.

Acha tutumie misemo ya Wahenga, ‘Kijua ndiyo hiki, usipoanika utautwanga mbichi’ cheza mpira kijana eleweka Feisal Fei Toto, ‘wakati ni ukuta’ na ‘Mechi hii siyo mchezo Fainali ipo uzeeni’ ….. ila Wahenga heshima kwenu.

Watano kizimbani kwa kujifanya Mawakala, kuibia watu
Maisha: Dawa ya kumtuliza mume ndani ya ndoa hii hapa