Mwamba anaitwa Sir Charlie Champlin (16 Aprili 16, 1889 – Desemba 25, 1977), alikuwa ni mwigizaji wa katuni wa Kiingereza na mtunzi wa filamu aliyejizolea umaarufu katika enzi ya filamu isiyo na sauti.

Alipata umaarufu ulimwenguni kote kupitia mtu wake wa skrini, Tramp na anachukuliwa kuwa mmoja wa watu mashuhuri zaidi katika tasnia ya filamu.

Kazi yake ilidumu kwa zaidi ya miaka 75, tangu utotoni katika enzi ya Victoria hadi mwaka mmoja kabla ya kifo chake mwaka wa 1977, na ilijumuisha sifa na utata.

Alifariki akiwa na miaka 88, akiacha ‘Statements’ nne matata ambazo zina msaada mkubwa sana katika maisha endapo utazitilia maanani.

1. Hakuna kitu cha milele katika dunia hii, hata matatizo yetu si ya milele.

2. Huwa napenda kutembea kwenye mvua, ili nikiwa nalia basi hakuna mtu anayeweza kuona machozi yangu.

3. Siku inayopotea sana maishani ni ile siku ambayo hatucheki.

4. Kuna Madaktari sita bora zaidi duniani (i) Jua, (ii) Kupumzika, (iii) Mazoezi, (iv) Chakula, (v) Kujithamini na (vi) Marafiki.

Champlin hakuishia hapo, anasema ukiuona mwezi, utaona uzuri wa Mungu na kiliona jua utaona nguvu za Mungu.

“Ukiona kioo, utaona uumbaji bora wa Mungu. Kwa hiyo amini. Sisi sote ni watalii, Mungu ndiye wakala wetu wa usafiri ambaye tayari ameweka ratiba, nafasi na mahali tunakoenda. Maisha ni safari tu,” alimaliza.

Bila shaka utakua umepata kitu maana maneno hayo ni wazi kuwa hayaponyi pekee bali pia yanajenga na kukupa morali katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Wasalaam.

Wataka tume kuchunguza vifo kwenye maandamano
Israel: Mkutano hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa ni kituko