Wanawake wameshauriwa kuwashirikisha wenzi wao wanapojiunga na vikundi vya huduma ndogo za kuweka na kukopa fedha VICOBA, ili waweze kushirikiana na kufanya maamuzi ya pamoja juu ya maendeleo ya familia.
Hayo yameelezwa na Mweka Hazina wa kikundi cha Super Women cha kuweka na kukopa fedha, katika kitongoji cha Unyakumi Kata ya Mandewa Mjini Singida, Asha Senge wakati wa uzinduzi wa huduma ya kuwasaidia watu wenye uhitaji katika jamii.
Amesema, Wanakikundi wamekubalina kuwashirikisha wenzi wao ili nao waunge mkono jitihada zao, na kwamba waliona vema kuweka fedha ndogo kila wanapokutana, na baada ya miezi mitatu wataitoa na kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.
Kikundi hicho, pia kimetoa nguo zikiwemo sare za shule kwa Watoto wawili, Mahindi kilo 36, Sabuni za kufulia na fedha zaidi ya Shilingi 100,000 ambazo ziligawiwa kwa wahitaji wengine watatu.

Picha: Wananchi wa Litola wafurika kumsalimia Rais Samia
Salaam za Rais Samia kwa maelfu ya Wananchi Namtumbo