Timu ya usimamizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais – TAMISEMI, imeendelea na ziara ya tathimini ya Huduma za Ustawi Jamii kwa kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na kuwaasa Wazee kufanya mazoezi ili kuimarisha Afya.
Rai hiyo imetolewe na Mratibu wa Dawati la Huduma kwa Wazee, Haroun Yunus kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Ustawi wa jamii Ofis ya Rais TAMISEMI.
Amesema, Wazee wanajukumu kubwa Sana katika malezi bora ya Jamii yeyote ile hivyo wanapaswa kisimamia wajibu wao kwa kutoa mafunzo bora kwa vijana kwa kushirikiana na viongozi wa dini.
Yunus pia ameisihi Halmashauri Kuendelea kuwatambua Wazee waliopo katika Halmashauri hiyo ili waweze kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa Wazee kama vile msamaha wa matibabu katika vituo vya Afya.
Akiongea kwa niaba ya Wazee hao Mwenyekiti wa Baraza hilo, Nemensi Sikazwe ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwatambua na kuthamini michango ya wazee katika ujenzi wa Taifa imara.
Katika ziara hiyo timu imetembelea Baraza la Wazee wa Kata ya Kasazama na kusikiliza changamoto zao mbalimbali ambapo pia timu imewaasa Wazee hao kuendelea kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha Afya zao.

Watatu wadakwa kwa ulaghai wa mapenzi
Ganga Zumba: Mwafrika aliyeunda ufalme wake Nchini Brazil