Wamongolia: Hawa ni wakazi wa Afrika ya Kati, wanaopatikana katika majimbo ya kusini ya Ikweta na Mashariki, majimbo ya Kaskazini ya Bandundu na jimbo la zamani la Kasai Mashariki (sasa Sankuru) huko Maniema na Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC.

Wanazungumza lugha ya Ngala na kulingana na vyanzo anuwai kadhaa ambavyo vimesaidia kufanikisha andiko hili, basi tunawapa kongole  watu wa Balolo, Bolongo, Lomongo na Mongos.

Wanazungumza pia lomongo na lahaja zake, lakini lingala hutumiwa sana na wakati mwingine huchukua nafasi ya lomongo kama lugha mama katika maeneo ya mijini.

Lakini pamoja na Waluba na Wakongo, wao wanaunda mojawapo ya makabila makubwa zaidi ya lugha mama za nchini DRC zamani ikifahamika kama Zaire.

Georges van der Kerken, aliwahi kuandika kuwa Wamongolia wanasemekana walitoka katika nchi ya kaskazini-mashariki ya Mto Nile, katika mikoa ya Ziwa Albert, Ziwa Edward na Ziwa Victoria la Afrika Mashariki.

Halafu akaandika kuwa wengine walikuja kutoka mikoa ya kaskazini zaidi kati ya miaka ya 1300 na 1500 (AD) na baadaye, wakafika eneo la Haut-Uélé, kisha Ikweta.

Hiyo inajumuisha koo kadhaa kama za Boangi, Bolia, Bokote, Bongandu, Ekondas, Mbole, Ndengese, Nkundo, Nkutu, Ntomba, Kole, Sengele, Songomeno, Iyasa, Bembe, Bakutu na Ngole.

Nyingine ni Wongo, Kuba, Kusu, Iyadjima (Iyaelima), Boyela. ,Sakata, Batetela n.k ambapo wote hawa wanadai kuwa na babu mmoja ambaye ni Mongo, ndipo pale ilipopelekra wakajiita Anamongo.

Huu ndio utofauti wa Taifa la DRC na wao huwa wanaufurahia sana uasili wao, hata uivyo wana haki maana ni vyema sana kujivunia kilicho chako si unajua tena Nyumbani ni Nyumbani hata kama kichakani, TUENDELEE KUJIVUJIA VYA KWETU.

Hezbollah wathibitisha kifo cha Nasrallah
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 29, 2024