Kundi la Wanamgambo la Hezbollah la nchini Lebanon, limethibitisha kifo cha Kiongozi wao Hassan Nasrallah aliyeuawa katika shambulizi la anga la Israel, Septemba 27, 2024.

Kufuatia kifo hicho, Hezbollah imeapa kuendeleza vita vyake ilivyovitaja kama niĀ  vitakatifu, dhidi ya Israel huku ikitamba kuendelea kuiunga mkono Palestina.

Awali, mara baada ya tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Israel, Luteni Kanali Nadav Shoshani aliandika katika ukurasa wa mtandao wa X kuwa “Hassan Nasrallah ameuawa.”

Hata hivyo, Jeshi la Israel lilisema Hassan Nasrallah aliuawa kwa shambulizi la anga, wakati wa mkutano wa Viongozi wa kundi hilo uliofanyika Dahiyeh, Beirut.

Marburg yauwa sita Rwanda, Waziri atoa tahadhari
Maisha: Tuendelee kujivunia vya kwetu