Waziri wa Afya wa Rwanda, Dkt. Sabin Nsanzimana ametangaza vifo vya Watu sita vilivyotokana na maradhi ya Marburg yaliyolikumba Taifa hilo.

Dkt Nsanzimana amesema ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya damu na maji maji kutoka kwa watu wenye maradhi hayo na kwamba inaweza kuchukua hadi wiki tatu kwa aliyeambukizwa kutoonesha dalili zozote.

“Wengi waliopoteza maisha na waliougua ni Wafanyakazi wa vituo hivyo vya afya,” alisema Waziri huyo wa Afya, Dkt. Nsanzimana.

Marburg unaoleta Homa kali uligundulika nchini Rwanda baada ya watu 20 kuripotiwa kuugua na wengine hawa sita kuthibitishwa kupoteza maisha.

Septemba 27, 2024 Wizara ya Afya ya nchi hiyo ilitangaza kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika vituo mbalimbali vya afya vya Rwanda na kutoa tahadhari kwa jamii kuwa makini.

Virusi vya Marburg vinafananishwa na vile vya vya Ebola, vikiwa vimegunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1967 nchini Ujerumani baada ya watu tisa kuambukizwa na saba kupoteza maisha.

Kweli Dunia imejaa maajabu, Karibu Ziwa Rosa - Retba
Hezbollah wathibitisha kifo cha Nasrallah