Hili ni Ziwa Rosa, pia linajulikana ndani kama Ziwa Retba, lipo kaskazini mwa peninsula ya Cape Verde, kaskazini mashariki mwa Taifa la Senegal.
Eneo hilo ni unmbali wa takriban kilomita 35 kutoka jiji kuu la Taifa hilo Dakar, likiwa na eneo la 3 km².
Ziwa hili linasifika kwa maji yake ya rangi ya waridi, ambayo huwa wazi aua huonekana hasa katika kipindi cha wakati wa kiangazi.
Rangi hii ya kipekee husababishwa na kuwepo kwa mwani wa Dunaliella salina, ambao hutoa rangi nyekundu baada ya ya kunyonya miale ya jua.
Kutokana na Chumvi nyingi iliyopo ndani ya maji ya Ziwa hilo, huwawezesha watu kuogelea na kuelea bila kuzama, kitu ambacho kinafanana na matukio ya Bahari ya Chumvi ambayo nayo watu huwa hawazami kutokana na mgandamizo huo.