Kutokana na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia nchini, Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH), imeanza kutekeleza maradi wa kuzuia vitendo hivyo kwa Wanawake na watoto wenye ulemavu.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa mradi wa chukua hatua sasa zuia ukatili, Glory Mbowe wakati akizungumza katika mafunzo ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto wenye ulemavu, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Amesema, “malengo mahususi ni kutoa elimu juu ya masuala ya ukatili na haki za binadamu, ili Wanawake na Watoto wenye ulemavu waweze kutambua haki zao za msingi lakini pia kuwajengea uwezo wanawake na watoto wenye ulemavu kuripoti vitendo vya ukatilii kwenye vyombo husika.”

Glory ameongeza kuwa, mradi huo ambao unatekelezwa katika katika Kata ya Buigiri, utatumika pia kutoa mafunzo ya namna gani watu wenye ulemavu watakqvyoweza kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Wilaya ya Chamwino, Malale Michael alisema moja kati ya vitu ambavyo wanawafundisha Wanawake na Watoto wenye ulemavu ni kujua maana ya ukatili.

“Tunawafundisha kwanza kujua ukatili ni nini lakini pia upo wa aina gani lakini wakisha jua nini ukatili wanawezaje kutoa taarifa za matukio ya ukatili ili vyombo husika viweze kuchukua hatua na kukomesha vitendo hivyo,” alisema.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Taasisi ya FDH, Joyce Mhana alisema kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya mwaka 1977 kila binadamu ni sawa hivyo hakuna sababu ya mtu kumfanyia ukatili wa aina yoyote.

Vifo watu 17: Tunachunguza tukio - Polisi
Wanawake changamkieni fursa sekta ya Madini - Mama Nakio