Polisi Nchini Afrika Kusini, imesema bado inafuatilia kujua sababu zilizopelekea vifo vya Watu 17, wakiwemo wanawake 15 ambao waliuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika matukio mawili tofauti.

Taarifa ya Msemaji wa Polisi wa Afrika Kusini, Brigedia Athlenda Mathe imeeleza kuwa msako bado unaendelea ili kuwatafuta na kuwakamata washukiwa wa tukio hilo lililoacha simanzi.

Taarifa hiyo imefafanua zaidi ikisema Wanawake 12 na Mwanaume mmoja waliuawa katika nyumba moja huku Wanawake watatu na mwanamume mwingine wakiuawa katika nyumba ya jirani na majeruhi mmoja kulazwa Hospitalini akiwa na hali mbaya.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani na visa vya mauaji ya watu wengi vimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 30, 2024
FDH waanza utekelezaji kupinga vitendo vya ukatili