Ni maarufu kwa jina la Mto Mwekundu wa Kusini na huitwa hivi ili kuutofautisha na Mto Mwekundu wa Kaskazini mwa bara la Amerika.

Ni Mto mkubwa uliopo Kusini mwa Marekani na ulipewa jina hilo kwa rangi ya maji yake mekundu kutokana na kupita katika nchi yenye oksidi ya chuma na miamba mingine ya sedimentary yenye madini.

Mto Mwekundu wa Kaskazini, wenyewe hutiririsha maji yake kati ya Minnesota na Dakota Kaskazini hadi jimbo la Canada la Manitoba ingawa hapo zamani ulikuwa tawi la mto la Mto Mississippi.

Mto Mwekundu ninaozungumzia hapa yaani ule wa Kusini wenyewe kwasasa ni tawi la mto la Mto Atchafalaya, ambapo mgawanyiko wa mto Mississippi ambao unatiririka hadi Ghuba ya Mexico ukiwa na muunganiko pia wa Mto wa Kale.

Unapatikana katika eneo la Vinicunca katika eneo la Cusco huko Peru ukiwa ni  moja ya maajabu ya asili kwa wanaotembelea eneo hilo la kupendeza.

Jambo hili la kipekee ni matokeo ya Milima ya Upinde wa mvua inayozunguka, inayojulikana pia kama Vinicunca au Montaña de Siete Colores, na Bonde Nyekundu.

Hata hivyo, wenyeji wanasema wakati wa msimu wa mvua, mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na mvua huosha mashapo yenye madini mengi ndani ya mto, na kutengeneza rangi yake nyekundu.

Mwonekano wake unaweza kutofautiana kutoka kwa kina kirefu, nyekundu hadi nyekundu laini, kulingana na viwango vya mvua vya hivi majuzi na wingi wa mashapo yenye madini mengi yaliyopo wakati wote.

Tofauti hii hufanya kutembelea Mto Mwekundu kuwa tukio la kusisimua na linalobadilika kila mara, rangi zake zinavyobadilika mwaka mzima pia huwa ni kivutio cha kutosha kwa Watalii.

Rais Samia azindua Kitabu cha Edward Moringe Sokoine
Wajadili ushirikiano uendelezaji Madini mkakati