Tanzania inakwenda kushuhudia mageuzi makubwa ya utunzaji wa mazingira, kupitia Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maryprisca Mahundi ameyasema ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati akihamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi na kuanza kupika kisasa kupitia nishati safi ya kupikia.
Amesema, “tunaposema tutunze mazingira, tunaweza kuona takriban hekta 469,000 za misitu zinateketea kwa mwaka sababu ya shughuli mbalimbali za binadamu ikiwemo matumizi ya nishati zisizo safi za kupikia (kuni na mkaa), hivyo tunapotumia nishati safi kupikia tunaenda kutunza mazingira yetu.”