Kisiwa cha alama za vidole.

Kinaitwa Baljenac au Bavljenac: ni Kisiwa kidogo kilichopo katika Bahari ya Adriatic karibu na pwani ya Croatia kwenye visiwa vya Sibenik.

Ni kisiwa cha takriban nusu maili ya mraba na kimefunikwa na safu ya kuta za mawe-kavu ambayo yanapoonekana kutoka juu ni kama alama ya kidole gumba cha binadamu.

Baljenac haina watu na sio mahali pekee ambapo kuta hizi za kipekee zipo, hata sehemu nyingi za mashambani za Croatia na Mataifa mengine ya Magharibi mwa Ulaya, kama  Ireland, Uingereza na Scotland, lakini kisiwa hiki kina upekee.

Umbo lake la asili lisilo la kawaida na maumbo kamili ya kijiometri, pamoja na mwonekano wa kuvutia wa angani, hukifanya kuwa mahali pa pekee, kiasi kwamba Serikali ya Croatia imeiomba UNESCO ikijumuishe katika orodha ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia.

Kuta za Kisiwa hiki, zilijengwa na Wakulima wa ndani katika miaka ya 1800, zikiwa zimeunganishwa pamoja na kama zingekuwa katika mstari mmoja basi zingekwenda umbali wa kilomita 23 (maili 14).

Arifu ya Bodi ya Kitaifa ya Watalii ya Croatia, inaeleza kuwa Kisiwa hicho kilitumiwa kwa kilimo na Wakulima wa kisiwa jirani cha Kaprije.

Walichofanya ni kufyeka ‘mimea mikali’ ya Baljenac, ili kutoa nafasi kwa mitini na michungwa, pamoja na mizabibu kisha kujenga kuta za mawe, ili kulinda mazao hayo kutokana na upepo, na kugawanya mashamba.

Kuta hizi za mawe zenye urefu wa kufika kiunoni, ziliundwa kwa kutumia mbinu inayojulikana kama ‘ukuta wa mawe makavu’, ambayo inahusisha kuweka miamba kwa uangalifu na kuingiliana.

Kongamano Jotoardhi kuyakutanisha Mataifa 13 Nchini
Iran yaipa vitisho vipya Israel, kisasi chatajwa