Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maziringira (UNEP), limeandaa kongamano la 10 la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) litakalofanyika nchini kuanzia Oktoba 21 hadi 27 mwaka huu.

Akizungumza hii leo Oktoba 2, 2024 jijini Dodoma, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mathew Mwangomba amesema  kongamano hilo linatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amesema, “litashirikisha washiriki kati ya 700 hadi 1,000 kutoka nchi 13 zikiwemo za Afrika, mataifa ya ulaya na uarabuni na litafunguliwa Oktoba 23, 2024 na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, likiwa na kaulimbiu inayosema, Kuharakisha Maendeleo ya Rasilimali za Joto ardhi katika Afrika, Masoko ya Gesi ya Ukaa na Upiunguzaji wa Gesi ya Ukaa.”

 

Mwangomba amesema, kaulimbiu hiy inasadifu azma ya Serikali ambayo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Wananchi wanatumia Nishati Safi ya Kupikia, kama ilivyoanishwa katika mkakati aliouzindua Aprili 2024 na kwamba mkakati huo una lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030.

Hata hivyo, amesema  kongamano hilo litaangazia mada mbalimbali ambazo ni uzalishaji umeme kwa kutumia joto ardhi, matumizi ya moja kwa moja ya joto ardhi katika sekta ya kilimo na ufugaji hasa wa samaki.

“Mada zingine ni uhandisi wa visima vya jotoa rdhi na teknolojia mpya, njia za kupata ufadhili wa miradi ya nishati mbadala ikiwemo nishati ya jotoardhi, uchambuzi wa faida za kimazingira na kijamii katika maendeleo ya miradi ya joto ardhi”,amesema

“Na pia mada zingine ni utafiti na uendelezaji wa rasilimali za joto ardhi, sera na udhibiti katika sekta ya rasilimali ya joto ardhi, faida ya kimazingira na kijamii katika maendeleo ya miradi ya joto ardhi”Amesema Mwangomba

Wataalamu wa Maabara toeni majibu sahihi - Dkt. Biteko
Malimwengu: Kisiwa mithili ya alama za Vidole