Washiriki wa Mkutano wa 53 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, wametakiwa kutumia jukwaa hilo kikamilifu kwa kuimarisha ushirikiano, kubadilishana mawazo bunifu na kuendeleza mikakati inayotekelezeka ambayo italeta manufaa makubwa kwa bara la Afrika na watu wake.

Wito huo, umetolewa hii leo Oktoba 3, 2024 na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Grand Melia, Jijini Arusha.

 

Aidha, alitumia fursa hiyo kuwashukuru wajumbe wa Umoja huo kwa kumchagua kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), huku akiwasihi kutumia uwepo wao mkoani Arusha kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii, ili kufurahia uzuri na urithi wa nchi ya Tanzania.

Mkutano huo, uliofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na umehudhuriwa na Maspika na Wabunge kutoka zaidi ya nchi 19 za Barani Afrika.

 

Tianmen: Muonekano wake umetengeneza uwezekano
Mhandisi Mramba asisitiza ufanisi huduma sekta ya Nishati