Watu wanne wamefariki dunia, na wengine 15 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya basi la Kapricon lenye namba za usajili T605 DJR, ambalo liliacha njia na kupinduka.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Maili kumi lililopo Barabara ya Segera-Korogwe.

 

Amesema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Dereva mkazi wa Arusha Julius Mushi (43), na lilipata ajali majira ya saa 7 na nusu, usiku wa kuamkia hii leo Oktoba 3, 2024 likiwa linatokea jijini Dar es Salaam, kuelekea Arusha.

Kufuatia ajali hiyo, Kamanda Mchunguzi amewataka Madreva kuendelea kufuata na kuheshimu sheria za usalama Barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Tianmen: Muonekano wake umetengeneza uwezekano