Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wadau wa lishe kuhakikisha wanatumia vizuri matokea ya ripoti ya mapitio ya muda wa kati, ili kujitathmini na kuchukua hatua stahiki za kuboresha utekelezaji wa afua za lishe.
Mjaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Kumi wa Wadau wa Lishe jijini Mwanza na kuiagiza Mikoa na Halmashauri zote nchini kutumia mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi wa elimu ya msingi.
Amesema, “hakikisheni matumizi ya vyakula vilivyorutubishwa yanajumuishwa na kutengewa fedha katika mipango na bajeti za kila mwaka. mikataba ya lishe kati ya Mheshimiwa Rais na Wakuu wa Mikoa itekelezwe kikamilifu na kuwa na tija. Endeleeni kufanya ufuatiliaji wa karibu na kutoa taarifa za utekelezaji mara kwa mara.”
Aidha, Majaliwa pia amezitaka Wizara, Wakala, Taasisi na Mashirika ya umma watumie kikamilifu mwongozo wa mpango jumuishi wa Taifa wa lishe na bajeti na kuhakikisha masuala ya lishe yanajumuishwa katika mipango na kutengewa fedha, ili yatekelezwe kikamilifu kila mwaka.