Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeendelea kulifanyia kazi suala la kodi kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kuijengea uwezo Mamlaka ya Mapato Nchini – TRA.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Septemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi.

Amesema, “Kufuatia mashauriano na wadau mbalimbali, serikali imeendelea kulifanyia kazi suala la kodi nchini. Tumeimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato na kuijengea uwezo TRA na kuimarisha mazingira ya kufanyia biashara nchini.”

Rais Dk. Samia ameongeza kuwa, uimarishaji huo wa mazingira ya biashara pia umeendana na ufutaji wa baadhi ya tozo na kuimarishwa kwa utendaji kwenye idara, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Malkia Yemisi: Mzalishaji wa Tani 10,000 za Mihogo, atoa somo
Kim naye atishia kuisambaratisha Korea Kusini