Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Jijini Dar es Salaam hii leo Oktoba 4, 2024 amesema Serikali itajenga mfumo wa kodi unaotenda haki, ambapo kila anayestahili kulipa kodi alipe kodi stahiki.
Amesema, kodi zote zitatozwa kwa mujibu wa sheria na kwamba unatakiwa mfumo wa kodi ambao utachochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuchangia ujenzi wa uchumi jumuishi unaoiwezesha Serikali kutimiza malengo yake ya kuleta ustawi kwa wananchi.
Amesema, “tunataka kujenga mfumo wa kodi unaotenda haki, ambapo kila anayestahili kulipa kodi alipe kodi stahiki, na kodi zote zitozwe kwa mujibu wa sheria. Pia tunataka mfumo wa kodi unaochochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na utakaochangia ujenzi wa uchumi jumuishi na unaoiwezesha serikali kutimiza malengo yake ya kuleta ustawi kwa wananchi.”