Mtangazaji Mkongwe na maarufu Nchini ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefariki dunia.

Dida amefukwa na umauti hii leo jioni Oktoba 4, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Alipata umaarufu mkubwa akiwa Radio Times FM ya jijiji Dar es Salaam kupitia kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani, kabla ya kuhamia kituo cha radio cha Wasafi Fm.

Atakumbukwa kwa harakati zake za kuujengea heshima Muziki wa Modern Taarab, Mduara, Mnanda na hata Singeli huku akiwa mahiri katika wa utangazaji.

PUMZIKA KWA AMANI MWANANCHI.

Habarikuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 5, 2024
Dkt. Samia: Tutajenga mfumo wa Kodi unaotenda haki