Historia imeandikwa Tanzania, baada ya Mkanda mwingine kubakia katika Ardhi ya Tanzania ambaoo Bondia Said Mohamed maarufu kama Said Chino kuwa bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship kwa kumchapa mpinzani wake raia wa Afrika Kusini Lusanda Komanisa kwa pointi.

Said Chino ameshinda pambani hilo kwa point kutoka kwa majaji wote watatu ambapo kwa ushindi huo Said Mohamed amezwadia #KnockoutyaMama ya Shilingi milioni tano kama zazawi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuisapoti sekta yote ya michezo na kwasasa mapambano yote ya kimataifa yatakayohusisha mabondia wa Kitanzania skiwa ni motisha kwa mabondia hao

#KnockoutyaMAMA

TKO ya Mafia heshima Tanzania, azoa Mil. 7 za Knockout ya Mama
Knockout ya mama: Amiri aipaisha Bendera ya Taifa