Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya Jijijini Dar es Salaam, imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob (Boni Yai)
Hoja hizo, zimekubaliwa hii leoOktoba 7, 2024 ambapo sasa Mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea.
Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Franco Kiswaga ametangaza maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi.
Boniface ameachiwa kwa masharti ya kuwa na Wadhamini wawili waliosaini bondi ya shillingi milioni saba, pamoja na kutotakiwa kusafiri nje ya Nchi bila taarifa na kesi hiyo kuahirishwa hadi Oktoba 21, 2024.

Maadhimisho EWW: Kagera watuma ujumbe Serikalini
Maisha: Usipobadilika fikra zitakubadilisha