Johansen Buberwa – Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa ametoa wito kwa Wananchi kutorusu wagombea ambao sio raia wa Watanzania kuchukua fomu za kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza na vyombo vya Habari ofisini kwake, RC Mwassa amesema Mkoa huo upo mpakani na wapo watu walioingia nchini na wengine wanaishi kinyume cha sheria ambao wangependa kuwa viongozi na wengine kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kutoa rushwa, ili wachaguliwe kuwa Viongozi.
Amesema, “Mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na idadi ya watu waliofikisha miaka 18 milioni 1,566,530 na kati ya hao wanawake laki 705,000 na wanaume laki 816,527.”
Mwassa amesemaVituo vya wapiga kura kwa mkoa huo vimeandalia 3,833 ambapo uandikishaji utaanza Oktoba 11 – 20, 2024 na zoezi la kuchukua na kurejesha fomu ni Novemba 1 – 7, 2024 kwa wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali.
Hata hivyo, Mwassa amesema Kampeni za uchaguzi zitaanza Novemba 20 – 26, 2024 na kawasihi wagombea wa vyama vyote vya siasa kutumia muda mzuri wa kufanya kampeini za kistarabu na zenyestaha za kunadi sera za vyama vyao ili kuwapa furusa wananchi kuchambua wachague viongozi wazuri wanao wataka.
Amewahakikishia wakazi wa mkoa huo kwamba uchaguzi huo wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024 utakuwa wa uhuru na haki na kwamba Serikali imejipanga kuratibu Zoezi hilo.