Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wa tukio la mauaji ya Mkazi wa Leguruki, Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha, Israel Paulo (36), aliyefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tengeru baada ya kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.

Tarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 9, 2024 na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Justine Masejo imewataja Watuhumiwa kuwa ni Ndewario Lazaro maarufu kwa jina Shombotoni (60), Mkazi wa Mwaruvango Wilaya ya Arumeru.

Mwingine ni Oscar Ndewario (29) mkazi wa Moivaro ambaye aliyekamatwa Wilaya Simanjiro Mkoani Manyara, aliyetoroka baada ya tukio.

Kamanda Masejo amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Kagera mwenyeji maadhimisho siku ya Chakula Duniani
Kikoti: Jamii iachane na matumizi holela ya Dawa