Johansen Buberwa – Kagera.
Mkoa wa Kagera unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo yatafanyika Oktoba 10 – 16, 2024 yakiambatanana maonesho mbalimbali, huku uzinduzi rasmi ukitarajiwa kufanyika Oktoba 13, 2024.
Hayo yamebaijishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajath Fatma Mwasa wakati akizungumza na Vyombo vya Habari ofisini kwake.
Amesema “siku hiyo watu watajionea na kujifunza kuhusu vyakula vya asili vinavyopatikana Mkoani humo sambamba na kutoa elimu ya lishe, ili kupunguza tatizo la udumavu kwenye jamii.”
Kwa upande wake Kaimu katibu Tawala Mkoa Kagera, Isaya Tendega amesema kwasasa unazalisha wastani tani milioni 3 na laki 4 na matumizi yake ni tani laki 7 na 70 na nyingine za ziada ya milioni 2 na laki 7 zinazouzwa nje ya mkoa huo.
Maadhimisho ya chakula duniani kwa mwaka huu wa 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo, “Haki ya chakula ya maisha bora ya sasa.”