Saikolojia ni nidhamu ya sayansi huru inayotumia karibia kila kipengele cha uzoefu wetu usio na mipaka ambapo Sayansi hiyo huzalisha maarifa kuhusu asili na ukuaji wa mawazo ya binadamu, hisia na tabia katika viwango binafsi na vya kijamii huku Wanasaikolojia wakifanya kazi katika mawanda mapana hasa pale ambapo utendaji kazi wa binadamu unahusika.

Sayansi ya saikolojia, huongeza ufahamu wa tabia ya binadamu katika muktadha wa kijamii, kiutamaduni na kilugha huku ikifahamika kuwa Wanasaikolojia wanao wajibu katika kusaidia afya na ustawi ulimwenguni katika muhimili wa haki za binadamu, kwa lengo la kuboresha maisha.

Wataalamu wa mambo ya Saikolojia na maumbile, wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu katika makundi makuu manne yaliyotengwa katika miundo mikuu miwili ambayo ni yale ya 1. Watu wenye uwezo mkubwa kiakili na jingine ni lile la 2. Watu walio na uwezo wa kawaida kiakili.

1: Watu hawa hufahamika kama Introvant, wenyewe wana uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina ambao hufahamika kitaalamu kama Melancolin na Fragmetic.

2: Wao hufahamika kama Extrvants, wao wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao na kitaalamu tunawaita Sanguine na Colerick.

MELANCOLIN

Ipo hivi, (i) Watu wa kundi hili (Wake kwa Waume), wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient), ni wapole na wasio na maneno mengi, wakiwa na hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati.

(ii), Watu hawa wana wajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida, matatizo au changamoto na inasadikika kuwa wao pia huwa waombaji au wanamaombi wazuri sana kiimani.

(iii), Watu hawa pia wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa, halafu kingine ni wagumu sana wa kusahau mambo yaliyowaumiza na hiyo imewasababishia kuwa wagumu pia wa kusamehe.

FLAGMETIC

(i), Watu wa aina hii wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin, uwezo wao ktk utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini.

(ii), Inaarifiwa kuwa hawa ni Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine ktk mambo yote na si watu wanaojali muda ama katiba.

(iii), Inasemekana watu hawa wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko na pia huwa hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao.

(IV), Watu hawa pia wanasamehe haraka sana kwa sababu huwa hawajali, ila ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera walizobainishiwa na wengine.

SANGUINE

(i), Wana uwezo wa kawaida kiakili na ni wacheshi sana wakiwa muda wote wana maneno mengi na wasiopumzika ingawa pia ni wavivu wazuri wa kazi.

(ii), Wana mipango isiyoona mbali, wakipenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha halafu ni kundi la watu walio na waoga na waongo sana huku tabia zao zikiwa ni za vinyonga.

(iii), Hawa jamaa kibaya zaidi si watunzaji wazuri wa siri halafu ni wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau na hupenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina halafu wanachukua kama akiba yao ya ufahamu bila kujali.

GOLERICK

(i), Wao wna uwezo wa kawaida kiakili lakini ni wakali na wakaidi wasio na huruma wala unyenyekevu.

(ii), Ni Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa na kwa kifupi ni madikteta.

(iii), Mara nyingi wana nguvu nyingi na si watu wanaopenda suluhu na amani.

MUHIMU

Sote tunafahamu tulivyo au kama si hivyo basi tunawafahamu watu wengine walivyo, hivyo kupitia ainisho hili sina shaka umeweza kugundua nani yupo katika kundi gani maana kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani au mojawapo kati ya hayo.

Kiuhalisia tunahitaji Wanasaikolojia kwa faida za kibinaadamu na kiuchumi na ni wazi kuwa hata Serikali zetu zinatakiwa zitambue mchango muhimu wa Wanasaikolojia katika kutuliza tabu au kuondoa mateso ikiwemo kuwezesha maisha kama msingi wa haki za binadamu.

Kwa tabia kama hizi baadhi ya Mataifa yameshindwa kushughulikia changamoto za afya ya akili kama vile Sonona na Wasiwasi ambapo aghalabu ni matokeo ya kupuuza viashirio vya kijamii vya afya na imegharimu uchumi wa dunia kwa kudhani yanaletwa na migogoro na kusahau kuhusu tabia za watu na jinsi ya kushughulika nao kisaikolojia.

Na ikumbukwe kwamba, Wanasaikolojia huwa wanaelewa tafiti za kibaolojia, kijamii na kimazingira na wamepata mafunzo ya kutumia mbinu zinazotegemea uthibitisho thabiti wa kuboresha maisha ya binadamu katika njanja za kiutamaduni na kilugha.

HITIMISHO

Ili kuwa mwanasaikolojia, muhusika lazima aoneshe weledi, sayansi, elimu ya maadili na ubora kwa kiwango cha juu, na hapa ndipo huwa mara nyingi namuangalia jamaa yangu Dupa wa Mdupange ambaye tayari ana maandalizi ya hali ya juu ya kuwa Mwanasaikolojia kwani hutilia mkazo wa kujitegemea kiutaalamu na kisayansi na wajibu wake huru kupitia nidhamu yake ya kuhamasisha ustawi wa mwanadamu katika kila eneo la maisha.

Watu kama yeye hufanya kazi kwa kutumia njia za kisayansi na kukamilisha ubainishaji wao wa matatizo, utambuzi, na ujuzi wa kufikiri kimantiki ambao hutoa njia ya kukamilishi hatma ya afya ya mwanadamu, kwani katika hii Dunia ya sasa yenye majanga mengi yasiyotarajia, mchango wa Wanasaikolojia katika kuondoa athari za kimwili, kihisia na kiakili kwa watu, makundi na jamii kama nilivyoainisha hapo juu ni muhimu sana.

Lakini hata hivyo naweza kusema kuna mambo ambayo ni kama tumechelewa kutokana na athari zake kwa jamii hivi sasa Duniani kote kutokana na kupuuza tabia kama za FLAGMENT, lakini ipo njia mbadala ya kuyakabili kwa kuanza na vizazi vya sasa kuvijenga kiimani na kielimu, ili kupata matokeo mazuri siku za mbeleni, kwani UKIPANDA DHARAU UTAVUNA KUDHARAULIWA, hakuna kushangaa.

Aliyepotea apatikana akiwa na majeraha, RC Sendiga atoa kauli
Kibaha: Shule ya Uongozi, Chuo Renmin kubadilishana wataalamu