Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkuuwa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka Wakala wa Mbolea na Wadau wa Kilimo Mkoani Manyara,  kusogeza huduma ya upatikanaji wa Mbolea Vijijini ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa bei ya ruzuku na kupata uhakika wa mbolea katika kipindi cha msimu wa kilimo.

Sendiga ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani na kudai kuwa Mawakala wengi wako mjini hivyo wanapaswa kusogeza huduma hiyo karibu na makazi ya watu Vijijini ili kuwapunguizia wakulima gharama.

Amesema, “Wafanyabiashara wanawajibu wa kusogeza mbolea kwa wananchi wanaohitaji mbolea,uwekaji wa mbolea kwenye miji,makao makuu ya Wilaya,makao makuu ya Mikoa hapo hakuna wakulima,wakulima wako Vijijini kwaio wafungue ofis za uwakala Vijijini ili kuwapunguizia wananchi mzigo mzito wa kuja kuchukua mbolea mijini na badae wanapata shida ya kusafirisha na mabasi.”

Aidha, Sendiga pia ametoa ombi kwa Mamlaka ya Uthibiti wa bei za mbolea Nchini kuona umuhimu wa kufanya mapitio ya bei elekezi, ili ziweze kuakisi uhalisia na miundombinu ya maeneo husika kwenye Mikoa mbalimbali.

“Na kwa hili ninaliwasilisha Ombi langu kimkakati kwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ili aweze kulichukua,Mkoa wangu ni Moja kati ya Mikoa ambayo imezagaa,jiografia yake ni ngumu sana kufikika,bei ikiwa Moja maeneo mengine wananchi wanashindwa kunufaika,” alisema.

Amesema,Viongozi katika ngazi ya Mkoa na Wilaya wahakikishe wanapitia na kuondoa changamoto zote za msimu zilizopita ili kuweza kuwahudumia wananchi kikamilifu ili waweze kunufaika katika sekta ya kilimo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uthibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema kupitia maonyesho hayo wananchi na Wakulima watapata fursa ya kujifunza matumizi sahihi ya mbolea pamoja na huduma nyingine za shughuli za kilimo ambazo zitaongeza uzalishaji wa tija.

“Mbolea huchangia kati ya asilimia 20 Hadi asilimia 40 na asilimia zingine zinazobaki zinategemea uzingatiaji wa kanuni Bora za kilimo,hivo tunaamini kupitia maonyesho haya wakulima na wadau wengine watajifunza matumizi ya mbolea kwa usahihi”.

Maadhimisho ya siku ya mbolea Duniani hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu Nchini Tanzania kitaifa yanafanyika Mkoani Manyara yenye kauli mbivu isemayo “Tuongee mbolea,kilimo ni mbolea”.

Maisha: Dawa ya Bosi anayechelewesha Mshahara
Ushirikiano: Balozi Kombo ateta na Rais wa Finland