Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wemejitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura katika maeneo mbalimbali, huku Wasimamizi na Mawakala wa Vyama vya siasa wakitahadharishwa kuheshimu na kulinda viapo vyao.
Wito huo, umetolewa na Diwani wa Kata ya Bakoba baada ya kushiriki zoezi la kujiandisha kwenye kituo cha Buyekera.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima ambaye naye alishiriki kujiandikisha amewahimiza wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza na kujiandisha, ili waweze kupata haki yao ya kimsingi ya kumchagua Kiongozi wao.
Naye Erick Bozompora ambaye ni Afisa Uchaguzi Manispaa Bukoba, amesema zoezi la uandikishaji kwenye daftari la mpiga kura katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ndani ya manispaa ya hiyo litafanyika kwa siku 10.
Amesema, katika kipindi hicho, Kata zote 14 mitaa 66 na vituo 82 vitaendesha zoezi hilo huku Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera, Naziri Karamagi akisema zoezi linaendelea vizuri mkwani amekua miongoni mwa waliohuisha taarifa zao.