Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ataitangaza siku ya Novemba 27, 2024 kuwa ya mapumziko, ili Watanzania waitumie kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
ambapo ameendelea kuwasisitiza Wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura ili wapate fursa ya kuchagua Viongozi kwenye maeneo yao
Akiongea na Wananchi wa Pasiansi baada ya kuwasili Jijini Mwanza leo Oktoba 12, 2024, Rais Samia amewasisitiza Wananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura, ili wapate fursa ya kuchagua Viongozi kwenye maeneo yao.
Amesema, “nawashukuru sana Wana Mwanza kwa makaribisho makubwa hivi, Airport nimekuta kumefurika, Viongozi wapo wengi nikajua ndio mapokezi yenyewe lakini RC akaniambia Wana Mwanza wanakusubiri Pasiansi wakukaribishe nawashukuru sana”
Aidha, Dkt Samia aliongeza kuwa, “mnajua jana tulianza zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga kura wa Serikali za Mitaa, Mimi nimejiandikisha niwaombe wengine twendeni tukajiandikishe wote na ile tarehe ikifika November 27, 2024 itakuwa Jumatano na nitaitangaza kuwa ni siku hamna kazi ili Watu wote kazi yetu siku hiyo iwe kupiga kura.”