Klabu za Simba na Yanga zimeendelea vyema na maandalizi ya Kariakoo Derby itakayopigwa tarehe 19 oktoba.Hii inakuwa dabi ya Kwanza kwa msimu wa 2024/25 ikiwakutanisha Simba waliocheza michezo 5 ya ligi kuu ya NBC wakishinda mechi 4 na sare 1 huku wakifunga mabao 12 na kuruhusu mabao 2 pekee na kuvuna alama 13.
Klabu ya Yanga imecheza michezo 4 ikishinda mechi zote na kufunga jumla ya mabao 8 wakivuna alama 12.
Taarifa kutoka Yanga na Simba zinasema wachezaji wamejiandaa vyema na mchezo huo wa kusisimua wenye taswira ya soka la Tanzania hivyo mashabiki wafike uwanjani kuushuhudia mchezo huo muhimu.
Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally amenukuliwa akisema “Tumejiandaa vya kutosha kukabiliana na mpinzani wetu,tunajua ubora wake na tunaheshimu hilo,historia haina nafasi kuelekea mechi hii. Benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamejitoa sana kuelekea mchezo huo mgumu na muhimu hivyo mashabiki wa Simba waje uwanjani kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa na wale wa upande wa pili waje kushuhudia maumivu kwenye mechi hiyo”
Naye afisa Habari wa Yanga amenukuliwa akisema “Tunaenda kufanya kile tulichokifanya msimu uliopita.Tuliwafunga nje ndani kwa magoli 7 na kwa ubora tulionao tunaweza kurudia hilo.Timu yetu iko imara na wachezaji wanamorali kuelekea mchezo huo. Silaha yetu ni ubora wa benchi la ufundi pamoja na ubora wa wachezaji wanaojitoa kila mchezo hivyo mashabiki wa Yanga wafike uwanjani kushuhudia timu bora Africa inavyokwenda kufanya maajabu.