Mwakilishi wa Wakili Peter Madeleka (Msimamizi wa kesi ya Paul Kisabo dhidi ya mtuhumiwa Fatma Kigondo ‘Afande’), Aaron Kishai amesema Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Nyambuli Tungaraja ametupilia mbali ombi lao kusaini hati ya kumsomea shitaka Mtuhumiwa (Afande) popote alipo, baada ya kubainika kuwa anaumwa hali iliyompelekea kushindwa kuhudhuria Mahakamani.

Akiongea na Vyombo vya Habari hii leo Oktoba 18, 2024 mara baada ya maamuzi hayo, Kishai amesema Hakimu Tungaraja ametumia kifungu cha 128 kifungu kidogo cha pili cha nne cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 kutosaini hati hiyo, akisema malalamiko hayo yana kasoro.

Amesema, “na amekuja na sababu kwamba kifungu cha 128 hakijaonesha ni kosa gani alilolifanya huyo mshitakiwa na kwenye ile ‘compleinant’ (mlalamikaji) kama mliiona kwa nyuma ile document (hati) haijawa filed (haiko kwenye utaratibu mzuri wa kutunzwa) na kwenye yale maelezo yameandikwa yule ‘victim’ (mwathiriwa) ilitakiwa afuate malekezo toka Mahakamani.”

Kwahiyo Mheshimiwa Tungaraja maelezo aliyoyatoa hii leo ni hayo, amesema yeye rufaa ipo wazi kwahiyo sisi ambacho tutakifanya ni kwenda Mahakama Kuu ili hatua zingine ziweze kuendelea, kwahiyo ni hayo yaliyojiri kwa leo, kesi naweza nikasema bado ipo maana mwenye maamuzi ya kutupilia mbali shauri hili ni DPP,” alibainisha Kishai.

Fatma Kigondo (Afande), anatuhumiwa kuwaagiza akina Nyundo na wenzake katika tukio la ubakaji wa Binti wa Yombo na hakuitikia wito wa Mahakama kwasababu zilizoelezwa kuwa anaumwa, hatua ambayo ilimfanya Wakili Madeleka kuiomba Mahakama isaini hati, ili mtuhumiwa huyo asomewe shitaka lake popote alipo.

Kenya: Kindiki apendekezwa kurithi mikoba ya Gachagua