Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendinga ametoa wito kwa jamii ya wachache ya wadzabe wilayani Mbulu kwenda kujiandikisha katika daftari la makazi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Sendiga ametoa wito huo katika kijiji cha Mongo wa Mono kilichopo kata ya Yaeda chini ilipo jamii ya Wahadzabe ambao maisha yao bado yanategemea uwindaji na kuokota matunda kama chakula, Sendiga amewataka wapate muda wa kujiandikisha, huku akiwapelekea zawadi hiyo ya kitoweo.

Baada ya kupokea zawadi ya kitoweo jamii hiyo ya Wahadzabe wameonesha kufurahia jinsi Mkuu huyo wa Mkoa alivyofika na kuwatembelea na kuahidi kuwa na utayari wa kujiandikisha.

Kongamano Tanzania, Iran laongeza fursa Kibiashara