Wizara ya Maji kupitia Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini ndio zenye dhamana yakuhakikisha huduma za maji safi na usafi wa mazingira zinawafikia wananchi wote katika maeneo ya mijini kwa viwango na ubora unaostahili.

Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini iliyowasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma imeeleza jitahada zilizochukuliwa katika kufikisha huduma hiyo kwa wananchi.

Moja ya vipaumbele vilivyo elezwa katika taarifa hiyo ni pamoja na kuongeza kasi katika ujenzi na ukamilishwaji wa miradi ya huduma ya maji na miundombinu ya majitaka pamoja na suala la upotevu wa maji.

Aidha, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Anna Lupembe amewapongeza watendaji na Wataalamu wa Wizara ya Maji na taasisi zake kwa kuendelea kufikisha huduma za majisafi katika maeneo ya mijini na vijijini.

Hon. Londo Sworn in as Ex-Officio Member of EALA in Kampala