Jeshi la Israel – IDF, kupitia mtandao wa X limechapisha taarifa inayothibitisha kuvishambulia vituo vya kijeshi nchini Iran, baada ya kutokea kwa milipuko sita katika mji mkuu Tehran na karibu na jiji la Karaj.

Kupitia taarifa hiyo, IDF imeeleza kuwa ilichukua hatua hiyo ikiwa ni majibu ya mashambulizi ya mfululizo yaliyofanywa na Iran na washirika wake wa kikanda tangu Oktoba 7, 2024.

Israel ambayo imekuwa ikipanga kujibu shambulizi la pili la makombora lililofanywa na Iran Oktoba 1, 2024 kutokea Iran katika kipindi cha miezi sita ilieleza kuwa, “Kama ilivyo kwa taifa lolote huru ulimwenguni, Taifa la Israel lina haki na jukumu la kujibu.”

Hata hivyo, awali Iran iliionya Israel dhidi ya kufanya shambulizi lolote, ikisema hatua kama hiyo dhidi ya Iran itajibiwa vikali huku Ikulu ya White House, ikisema mashambulizi haya ya Israel nchini Iran ni hatua ya kujilinda.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 26, 2024