Idadi ya vijana wanaoumwa saratani nchini Kenya inazidi kuongezeka, ambapo takwimu zinaonyesha karibu vijana laki moja wanaugua ugonjwa huo, huku Wahudumu wa afya wakilihusisha ongezeko hilo na uzingatiaji duni wa lishe bora.
Taarifa ya Muungano wa Mashirika ya Saratani nchini Kenya, inaeleza kuwa takwimu za sasa za maradhi ya saratani miongoni mwa vijana ni virusi vya HPV vinavyosambazwa kwa ngono.
Aidha, virusi hivyo pia vinahusishwa na ongezeko hilo huku wakitoa wito kwa vijana kuwa makini katika mahusiano yao ya kimwili na kuzingatia njia bora za lishe ikiwemo kufanya mazoezi.
Kufuatia hali yo, Wahudumu wa afya wamesema kuna umuhimu wa kuendesha uhamasishaji miongoni mwa vijana ambao mara nyingi hawaamini kuwa wanaweza wakapata saratani wakidai ugonjwa huo ni wa watu walio na umri mkubwa.