Swaum Katambo – Katavi.

Vijana Mkoani Katavi, wametakiwa kukubali kukusanywa na kuwekwa pamoja, ili kupewa elimu ya ujasirimali itakayo wasaidia kujikwamua kiuchumi na kuepuka maneno ya kulelewa na wamama wakubwa (MASHANGAZI).

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Katavi Onesmo Buswelu katika maadhimisho ya wiki ya Mwanakatavi ambapo alipata nafasi ya kutembelea viwanda mbalimbali vya uzalishaji nakuwataka vijana kuiga mifano ya waliofanikiwa.

Amesema, “hebu tutoe wito kwa vijana wakubali kukusanywa, kuwekwa pamoja, wakubali kupewa elimu alafu waijaribu hiyo elimu kwenye maisha itawatoa.”

“Vijana wa kiume wasitake kwenda kulelewa na wamama wakubwa washangazi,vijana wa kike wasikubali kuzulula mtaani kusiko eleweka,” aliongeza DC Buswelu.

LEONBET kuwatajirisha watakao bashiri matokeo ya Trump, Kamala
Maisha: Waliopora mamilioni wakutwa wameganda