Mashambulizi mawili tofauti ya roketi za Hezbollah, yamewauwa watu saba katika eneo la kaskazini mwa Israel, huku mamlaka zikisesema ni siku mbaya zaidi ya tukio hilo kuwahi kutokea katika kipindi cha hivi karibuni.
Roketi hizo, zilitua karibu na mji wa Metula uliopo kwenye mpaka na Lebanon na kusababisha vifo vya Watu hao ambao ni Mkulima wa Israel, Wafanyakazi wanne wa kigeni wa Kilimo, Mwanamke wa Kiisraeli na mwanaye waliokuwa katika shamba la Mizeituni karibu na Kibbutz Afek, nje kidogo ya mji wa pwani wa Haifa.
Hezbollah ilisema imerusha makombora kuelekea eneo la Krayot Kaskazini mwa Haifa, na kwenye ngome ya vikosi vya Israel vilivyopo kusini mwa mji wa Lebanon wa Khiam, nje ya mpaka wa mji wa Metula.
Jumla ya makombora 55 yalirushwa kuelekea eneo la Magharibi mwa Galilaya iliko katika miji ya kibbutz , Galilaya ya Kati na Galilaya ya Juu mapema hapo Oktoba 31, 2024 mida ya alasiri.
Hata hivyo, Jeshi la Israel limesema baadhi ya makombora yalidunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga, huku mengine yakianguka katika maeneo ya wazi bila kuleta madhara.